Tuesday, 20 May 2014

News: Q-chillah aeleza kilichotokea kabla ya kifo cha director mashuhuri Adam kuambiana walipokiwa wlocation


Msanii wa Bongo Flava ambaye anajihusisha pia na uigizaji, Q Chief au Chillah ambaye alikuwa mmoja kati ya watu waliokuwa location na Marehemu Adam Kuambiana wakishuti filamu ya ‘Jojo’, ameelezea kilichotokea kabla ya kifo cha Adam Kuambiana.
 
“Tulikuwa kambini tunashuti movie yake mpya ambayo inaitwa Jojo, movie ambayo yeye mwenyewe alikuwa anasema itakuwa ni movie ya mwisho kwake. Ni movie ya mwisho kwa muda huu na atakaa kama miaka mitatu kuangalia vitu vingine halafu atarudi. Atakuwa tu ana-direct hatocheza.”Amesema   Q Chillah
 
Ameeleza kuwa tayari walikuwa wameshashuti filamu hiyo Bagamoyo, Iringa na muda huo walikuwa Dar es Salaam ambako walikuwa wanashuti scene za mwisho.
 
“Leo asubuhi tulikuwa tunaingia location pale biashara complex. Na wakati tunaingia location mimi najitayarisha kuoga. Assistant director wa Adam ambaye anaitwa Muxin, akanipigia simu ‘bana Adam yuko hotelini, yuko chumbani huku lakini simuelewi’. Mimi naingia nakuta Adam yuko Chooni anaharisha. Tukajitahidi kumwagia maji lakini anaahisha damu.”
 
Ameeleza kuwa waliamua kumbeba na kumkimbiza hospitali ya kwanza ambayo walikataa kumpokea kutokana na hali yake.
 
“Tukasema tutoke twende hospitali ya pili. Tumeenda private, kufika private daktari anamuangalia within 10 minutes tunajaribu kutafuta simu kupigia mkurugenzi wetu, kuwapigia watu wa Bongo Movies najaribu namba ya JB kumbe hayupo…Doctor anasema ‘huyu mtu hatuko nae tena, mwili umeacha roho’.” Q Chillah amesimulia kwa majonzi.
 
Ameongeza kuwa kuna filamu nyingi sana Tanzania ambazo jina la Adam Kuambiana limesaidia kuzikamilisha na kwamba tasnia ya filamu imepoteza mtu muhimu sana.
 
Mwili wa marehemu Adam Kuambiana umepumzishwa kwenye makazi ya kudumu leo Jumanne (May 20,2014).
 

0 comments:

Post a Comment