Thursday, 8 August 2013

UPCOMING MC: MFAHAMU CHALI ANAEKUJA KWA KASI KWENYE GAME HILI LA BONGO HIPHOP.



Dogo anaekuja kwa kasi kwenye Game akitambulika kwa jina la YOUNG KACHA a.k.a Mr. Dear Facebook au unawezamuita kaka wa YOUNG KILLER kutokana na kutoa remix ya dear Gambe na kufanya poa sana zaidi ya dear gambe. Dogo huyu pia ametoa ngoma kali zaidi aliyomshirikisha DARASSA na kijana toka Kenya aitwae MILLTANA...
Sasa anawaomba mashabiki wake wakae ule mkao wa kula kutokana na project kali anayoiandaa. Hivi karibuni amekuwa akikesha studio na yule tajiri wa EBSS wa mwaka jana hapa nikimzungumzia WALTER CHILAMBO wakiandaa project hiyo ambayo hutakiwi kabisa kucheza mbali na mchongo huo!


Hizi ni kati ya ngoma toka kwa Young Kacha.

Young Kacha ft. Darassa & Milltana-Traveller




Young Kacha-Dear Facebook


0 comments:

Post a Comment